Monday, 5 October 2015

Davido atangaza tarehe mpya ya kuachia Album yake

Davido ametangaza tarehe mpya ya kuachia Album yake ‘Baddest’ ambayo ilishindikana kutoka mwezi wa 9 kama alivyokua ameahidi awali.

Mwenyekiti wa Label ya HKN record inayomsimamia Davido, Adewale Adeleke amesema Album hiyo iliyowashirikisha wasanii wakubwa wa Marekani kama MeekMill, Trey Songz, Akon itatoka Jumamosi ya tarehe 10 October.

davido 

Mara ya kwanza Album hiyo ilipangwa kutoka June 8, lakini ilisogezwa tena hadi August 8 ambapo pia ilishindaka na kusogezwa hadi mwezi wa 9 ambao umepita kimya kimya mpaka sasa imepewa tarehe mpya October 10.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment