Mwezi May mwaka huu tulifahamishwa kuwa Said Fella kupitia kituo chake cha Mkubwa na Wanawe Youth Center, anawajengea nyumba za kisasa wasanii wanne wa kundi la Yamoto Band zitakazokuwa sehemu moja (Ingiahapa).
Kiongozi wa Yamoto Bnd, Aslay Isihaka amesema kuwa nyumba hizo ambazo
ameziita ‘kijiji cha Yamoto’ kutokana na kujengwa sehemu moja na kwa
kufanana, zimekaribia kukamilika.
“Vile vitu ambavyo tulikuwa tunavificha ficha sasa hivi vinakaribia
kumalizika,” alisema Aslay kupitia kipindi cha Friday Night Live cha
EATV Ijumaa iliyopita. “kwahiyo alhamdulillah sasa hivi mambo yanakuwa
mazuri kidogo, tuseme tuna kijiji chetu Yamoto Band, soon nafikiri blaza
(Sam) utachukuliwa utaenda utaambiwa hiki ndio kijiji chao Yamoto
Band”.
Wazo la nyumba hizo kujengwa sehemu moja lilitolewa na Aslay, na Fella alilipitisha na kuanza kulifanyia kazi.
Yamoto Band inaundwa na waimbaji wanne ambao ni Aslay, Maromboso, Beka na Enock Bella.
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment