Mtandao maarufu wa kushare picha wa Instagram ume‘verify’ akaunti ya Diamond Platnumz na kumfanya aingie kwenye orodha ya wasanii wa Afrika akiwemo Davido, wenye akaunti zilizokuwa verified.
Akaunti ya Diamond imekuwa verified na kuwekewa kitiki cha blue kuonesha
kuwa ni akaunti halali baada ya kufikisha followers 1.1 million, na
kumfanya awe ni msanii ambaye akaunti zake zote tatu za mitandao ya
kijamii Facebook, Twitter na Instagram ziko verified.
Baba Tiffah na uongozi wake wameondoka Tanzania kuelekea Milan, Italy
kwenye tuzo za MTV EMA 2015 zitakazotolewa Jumapili ya October 25 siku
ambayo Watanzania watakuwa wakipiga kura kumchagua Rais na wabunge.
Leo Oct.24 saa 6 usiku ndio itakuwa mwisho wa kupiga kura za MTV EMA,
hivyo bado hujachelewa kumuongezea Diamond kura yako ili kumuhakikishia
ushindi wa tuzo ya ‘Best World wide Act’ akiwa ni mwakilishi pekee wa
Afrika nzima.
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment