Sunday, 16 August 2015

Sauti Sol watangaza kuachilia ngoma hivi karibuni waliyo ifanya na Ali Kiba


Sauti Sol wanamuziki kutoka nchini Kenya ambao wanavuma kimuziki kutokana na ngoma zao kali ikiwa ni pamoja na Sura yako, Nerea waliyo mshirikisha Amos na Jos , Wametangaza kuachilia ngoma ambayo wameifanya na msanii wa Tanzania aliye shinda Kili Music Award 2015 tuzo tano Ali Kiba.

 

Saut Sol wamezungumza hayo kwenye show inayoruka live kila siku ya Ijumaa saa nne kamili usiku hadi saa sita kamili usiku EATV-Friday Night Live, pale walipo hojiwa na mtangazaji wa show hiyo Sam Misago kuwa kwa Tanzania wanaweza kufanya collaboration na msanii yupi?

 

Mbali na kufanya collaboration na msanii Ali Kiba, Saut Sol wamesema pia kwa Tanzania wasanii ambao tutarajie kuona wakifanya naye collabo wamesema ni Vanessa, Fid Q, Weusi na pia Feza ambaye alikuwa pia kwenye show ya FNL.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment