Wednesday, 27 May 2015

Meek Mill akanusha uvumi wa kumvalisha Nicki Minaj pete ya uchumba, Na kusema bado sana kuja kufanya hivyo

Uvumi wa Nicki Minaj kuvalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa sasa 'Meek Mill' ulianza kuvuma mwaka huu mwezi wa nne pale ambapo mwana hip hop Nicki Minaj alipo share picha Instagram ikionyesha pete yenye nakshi nyingi akiwa kaivaa kwenye kidole cha shada.

Lakini kwenye mahojiano aliyo fanyiwa Meek kwenye The FADER, Yeye binafsi amekanusha kufanya hivyo nakusema kuwa bado muda rasmin wa kufanya hivyo kwakuwa bado anataka kumfahamu zaidi Nicki Minaj na kujua hasa hisia zake ziko namna gani ili yasije kuwa mapenzi ya kuumizana hapo baadae.
“But it ain’t really time to get married yet. We’re still learning each other, feeling each other out.”

Kitendo cha Nicki Minaj kuonyesha pete hiyo Instagram na Meek Mill kuonyesha comment ya love kiliwafanya wengi kuwapa hongera hata marafiki wa karibu akiwemo Drake.
Wapenzi hawa wanatarajiwa kuwa karibu zaidi hasa kwenye Tour anayo tarajia kuifanya Nicki Minaj iitwayo 'Pinkprint Tour' mwezi July.

credit : tubongetz

FOLLOW US ON

No comments:

Post a Comment