Fid Q na Joh Makini ni marapper ambao wamekuwa wakichukuliwa kama hawaivi chungu kimoja, na wakati mwingine wamekuwa wakishindanishwa na mashabiki wanaotaka kujua nani mkali zaidi ya mwenzake.
Fareed “Fid Q” Kubanda ametoa mtazamo wake wa kile anachodhani kuwa sababu ya mashabiki wa muziki wa Hip Hop kumshindanisha na rapper mwenzake Joh Makini kwenye mitandao.
“Labda ni kwasababu (Joh) anaweza akawa
ni msanii ambaye anafanya vizuri kwahiyo wanakuwa wanamshindanisha na
msanii mwenzake mwingine (Fid) ambaye anafanya vizuri, lakini sidhani
kama kuna kitu personal na siko katika position kuamini mi nahitaji
kushindanishwa na Joh.” Alisema Fid kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
Fid amesema kuwa yeye ni msanii ambaye
hawezi kushindanishwa na msanii mwingine yeyote kutokana na kile
anachokifanya kuwa tofauti na wanachofanya wasanii wengine wote, na pale
anaposhindanishwa huwa anaona kama amedharaulika.
“Nadhani wanaoshindanisha wajifunze kuwa
wanafatilia watu wanaotaka kuwashindanisha kwanza, mi nadhani niko
tofauti kidogo na wanamuziki wengi sana ambao wanafanya Hip Hop na hiyo
haijalishi kama ngoma zangu zinapigwa sana redioni au hazipigwi.
Kibongobongo kiukweli mi sidhani naweza
kushindanishwa na mtu na wala siwezi kujisikia vizuri, na mara nyingi
naposhindanishwa na mtu naona kama nimedharaulika hivi, sio kwasabbu
huyo mtu mwingine ni dhaifu No!, kwasababu mi nafanya kitu cha tofauti
sana…nazingatia zaidi uandishi, nafanya show mpaka kesho na ngoma kama
dotcom, dotcom ni ngoma ambayo nimeitoa 2003, 2004.
Katika show zangu hizo hizo napigaga
Mwanza Mwanza ambayo imetoka 2005 ilikuwa nyimbo bora ya Hip Hop…saizi
ni 2015 tunaongelea miaka tisa iliyopita na zaidi, basi hebu tuangalie
basi na hao wengine ambao wanataka kunishindanisha nao wana vibao vyao
vina miaka hiyo tisa ambavyo wanaweza kufanya sasa hivi vingapi?”
Kuhusu kama amewahi kuwa na matatizo yoyote na Joh Makini:
“Sijawahi kuwa na matatizo na Joh
Makini, nadhani matatizo yanayosikika kwa watu unajua fans wana vitu
vyao, ukiingia sehemu mara utakutana na mtu kaweka picha sijui Fid Q vs
Joh Makini nani noma, nadhani vitu kama hivyo ndo waga vinatengeneza
chokochoko nyingi nyingi ambavyo mtu kama sio mtu wa kufikiria vyema
unaweza kuchukulia personal.”
No comments:
Post a Comment