Saturday 11 April 2015

Mo Music kuachia Mkwaju Mpya J3

Baada ya ukimya wa muda mrefu hit maker wa ‘Basi Nenda’ Moshi “Mo-Music” Katemi anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Nitazoea’.

Wimbo huo ambao utakuwa ni single ya nne kwa msanii huyo kutoka jiji la miamba Mwanza utatoka Jumatatu April 13.

‘Nitazoea’ ni wimbo wa Mapenzi ambao umetayarishwa na ma-producer watatu ambao ni Aby Daddy, Lollipop na D-Classic.

video ya ‘Nitazoea’ itaanza kufanywa wiki ijayo na Adam Juma wa Next Level.
Nyimbo za Mo Music zilizopita kabla ya huu ni ‘Basi Nenda’ ambayo ilifanya vizuri kila kona ya nchi, na kufuatiwa na ‘Simama’ pamoja na Almasi ambazo zilitoka kwa pamoja mwishoni mwa mwaka jana.

FOLLOW US ON


No comments:

Post a Comment