Wasanii ambao waliwahi kuwa wapenzi rapper Isaack Waziri “Lord Eyez” Makuto na muimbaji Rehema “Ray C” Chalamila hivi karibuni watasikika kwenye ngoma waliyofanya pamoja.
Lord Eyez ameiambia Clouds Fm kuwa wimbo huo ambao amemshirikisha ex-wake Ray C unaitwa ‘Matatizo’ umefanywa kwenye studio ya Mandugu Digital chini ya producer aitwaye Shaqee.
“Ngoma imeelezea mambo mengi kuhusu maisha kama jina linavyojieleza imeshakamilika kila kitu nitaitambulisha hivi karibuni kwenye kipindi cha xxl,”alisema Lord Eyez.
Mwaka jana (2014) Ray C alionesha nia ya kutaka kumsaidia Lord Eyez kwa kumshauri abadili mwenendo wa maisha yake na aachane na matumizi ya dawa za kulevya yaliyokuwa yakimsababisha rapper huyo kuingia kwenye majanga kila mara, pia alimkaribisha kutumia tiba ya Methadone (Ingia hapa).
Credit : Bongo5
Credit : Bongo5
FOLLOW US ON
No comments:
Post a Comment