Friday, 17 April 2015

Ali Kiba yuko Chimbo akipika Album Mpyaa.

Muimbaji wa ‘Chekecha Cheketua’ Alikiba a.k.a King Kiba kwa sasa hafanyi collabo na wasanii wengine na ametoa sababu iliyomfanya achukue uamuzi huo.


Akizungumza kupitia Leo Tena ya Clouds Fm, Alikiba amesema amechukua uamuzi huo kwasababu anamalizia kurekodi album yake ambayo iko kwenye hatua za mwisho.
“Nimestop kufanya collabo, sababu namalizia kazi zangu flani namalizia album nikimaliza ntaendelea kufanya featuring.” Alisema Alikiba.
Msanii mwingine wa Afrika ambaye amechukua uamuzi kama wa Kiba ni Davido, ambaye mapema mwaka huu pia alitangaza kusitisha kufanya collabo ili amalizie album yake.
 
FOLLOW US ON

No comments:

Post a Comment