
Takribani miezi mitatu imepita tangu Chidi Benz azungumzie kuhusu harakati zake za kufanya album na mkali wa hip hop Fid Q, Fareed vs Rasheed. Leo hii Ndani ya XXL ameongelea alipofikia juu ya kukamilisha album hiyo
Album hiyo ambayo imetokana na idea ya Chidi Benz tayari imeshaanza
kufanyiwa kazi ambapo ngoma moja imeshakamilika lakini Chidi pia
ameongelea kuhusu yeye mwenyewe na ratiba ya kuingia studio.
"kwasababu tulisha record ngoma moja so nafkiri sasa, now tunatakiwa
tuingia mzigoni so nahisi the project itakuwa noma and me najitayarisha
kuingia ingia vistudio napitia vistudio viwili vitatu hapa na pale nini,
kwahiyo natafuta bado, nahisi nikijakupata msumari ntakuja tu kusema
jamani eeh baada ya huu ni huu sasa hivi niko nautengeneza tengeneza na
create," amesema Chidi
Ya tunafanya album mzima inabidi tupge mikono tu, chidi na fid kwasababu
ni Rasheed na Fareed kwahiyo tumeamua tu sisi wenyewe kufanya
kitu..........
Ni idea yangu nilikuwanayo kabla sijatoa ngoma wala sikujua kama
nitakuwa busy na ngoma kwahiyo nilikuwa najua kwamba kwa kipindi ambacho
nitakuwa nimekaa nirecord project na Fid so ya imekuja imekuwa ratiba
imebaki pale pale tunafanya, tuna mpango tu wa kupiga ngoma za ajabu
sana." alimalizia Chidi
No comments:
Post a Comment