Tumezoea kuona filamu za nje kama"Step Up " na "Stomp the yard " zinazo
onesha masuala ya dance lakini kwa mara ya kwanza Msanii wa Bongo movie Irene
Uwoya na Msanii wa Bongo Flavour Msami wamefanikiwa kukamilisha filamu yao ya
kwanza ikiwa na maudhui kama ya filamu hizo za nje lakini ikihusisha zaidi aina za
dance za Afrika , Ireneuwoya ndio aliemtambulisha Mpenzi wake Msami
kwenye kiwanda cha bongo movie na ndani ya muda mfupi wawili hao tayari
wamefanya kitu kikubwa kinachoweza badilisha tasnia nzima ya filamu Tanzania ,
Msami alipokua akihojiwa na kipindi cha XXL cha clouds fm alifunguka kuwa filamu hiyo
itahusu masuala ya Dance na aliongeza kuwa filamu hiyo imefanyika nchini South
Africa na baadhi ya scene zimeigiziwa nchini uturuki pia sura za wakali wengine wa
Bongo Movie kama Mzee Majuto zitaonekana ndani ya filamu hiyo . Wapenzi wa Filamu
wakae tayari kwa kitu hiki cha tofauti na kipya kutoka kwa Sexylady Irene Uwoya na
Msami bab,
Zidi kuwa Nasi Tutakupa Trailer Ya Movie Hiyo Hapa Hapa
Zidi kuwa Nasi Tutakupa Trailer Ya Movie Hiyo Hapa Hapa
No comments:
Post a Comment