Tuesday, 30 September 2014

Hivi ndivyo Said Fella alivyoangaika Mpaka shaa kuanza kulipwa kupitia Youtube

Meneja mkongwe na muewezeshaji wa Mkubwa na Wanae, Said Fella amefunguka kuhusu njia alizotumia kutafuta nafasi ya biashara ya wasanii wake akiwemo ‘Shaa’ kulipwa pale kazi zake zinapowekwa YouTube.

Fella amesema yeye na Babu Tale waliumiza kichwa baada ya kuona wasanii wa Kenya wanaingiza pesa hata kama hawajatoa wimbo mpya, bila kutegemea shows na ndipo walipoamua kusafiri hadi Nairobi kuhakikisha wanafahamu nini hasa cha kufanya.

“Kweli tukaenda Kenya, tukaenda kukutana watu tukawauliza ‘jamani nyie mnaendaje mbona sisi tukiwapelekea wenzetu wanaotuuzia ringtone hapa Tanzania hatupati faida ile’. Lakini unakuta Jua Cali au Nyota Ndogo kafanya muziki zamani lakini anaendelea kula faida.” Amesema Said Fella.

“Yaani tumesafiria tobo na ndio maana tumelipata tobo. Hata juzi kati Babu Tale na Diamond walivyoenda Nigeria kwenda kusaka tobo…na ndio maana tunasema timu yetu Saka Tobo ili kwenda kuangalia wenzetu wanafanya nini na tunakwenda wapi. Kwa hiyo huwezi kumfuata tu mtu ukamwambia ebwana tobo hili…waje tuwaoneshe. Watanzania tunapendana.” 

Said Fella aliyasem ahayo alipokuwa akihojiwa na Times Fm

Shaa ambaye kimuziki anasimamiwa na Said Fella hivi sasa analipwa kwa kazi anazoweka kwenye channel ya YouTube.

Video yake ‘Sugua Gaga’ imevunja rekodi ya video za bongo flava kwa kuangaliwa zaidi YouTube, 

No comments:

Post a Comment