Tuesday 22 September 2015

Wizkid aahirisha tena kuachia album mpya mpaka mwakani (2016)!

Mashabiki wa Wizkid waliokuwa wakisubiri kwa hamu album mpya ya staa huyo ambayo ilipangwa kutoka Septemba, watalazimika kuvuta tena subira hadi mwakani 2016.

Wizkid ametangaza kusogeza mbele tarehe ya kuachia Album yake baada ya kuhudhulia sherehe ya kuzaliwa ya 2face Idibia aliyefikisha umri wa miaka 40, amesema sababu za kusogeza mbele ni kwa ajili ya kujipanga zaidi kutokana na mambo mengi aliyojifunza kutoka kwa 2 face.

 
Wizkid akiwa na 2 face

Hata hivyo Starboy ameahidi kuachia EP (extended play) yenye nyimbo 10 pamoja na video mwezi October mwaka huu.  

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment