Tuesday 22 September 2015

Diamond asema 'mashavu' kwa Tiffah hayajaja yenyewe tu, ni ubunifu wake

Makampuni makubwa hayajatangaza kupitia picha za kwanza za Diamond Platnumz, Latiffah hivi hivi. Kwa mujibu wa staa huyo ni ubunifu wake na proposal nzuri ndizo zimeyavutia.

Diamond ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM jana 21/9 kuwa yeye binafsi amepigana kuangalia mwanae atapata vipi deals zitakazomwingizia pesa.

“Wakati mwingine kama mzazi wasanii na celebrity lazima tuangalie tunajiongunisha vipi na makampuni. Tusiwe tunayalaumu tu makampuni haya support wasanii, lazima na wewe uwe creative,” amesema. “Uwe mzuri wa kuandika idea na kupeleka kwa watu tofauti tofauti.”

 
 
Aliongeza, “sisi tumepeleka na tukaifanyia presentation, wakasikiliza wakaona ina faida kwetu na kwao pia. Let’s say mtoto wako akiwa ni balozi wa bima ya kampuni yako itaongeza watoto kwa sababu kila mtu atajua kuna umuhimu gani wa mtoto kuwa na bima ya afya.” 

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

 

No comments:

Post a Comment