Wednesday 23 September 2015

"Viva Roma Viva haijafungiwa, inabaniwa tu" Roma Afunguka


“Kiukweli mimi kama artist nipo dilemma, kwa sababu kwa utaratibu kama msanii akiachia nyimbo anasambaza katika radio station, unapopeleka nyimbo yako katika vituo vya redio baadaye utataka feed back ngoma yako imepokelewaje, imepita na inachezwa na watu wameipokeaje? Kwahiyo baada ya Roma kufanya hilo zoezi si kila media ilipokea nyimbo na ikaipiga. Kila redio ilikuja na jibu lake tofauti kwamba, hii nyimbo hapana hatujaruhusiwa kama kituo cha redio kuipiga. Wengine wakasema tunaicheza lakini hatutaicheza tena kwa sababu ina maneno fulani hivi makali sana,” - Roma.

“Na wengine wengi wanaipiga mpaka sasa hivi na imeshaingia kwenye chati mbalimbali za redio. Lakini lile tamko rasmi kwamba nyimbo imefungiwa mimi sijapata kutoka kwenye mamlaka fulani husika zaidi baadhi ya redio zinasema nyimbo yako imefungiwa, ukienda kwingine sisi tunaicheza,” aliongeza Roma. 

Kwa upande mwingine Roma amesema video ya wimbo huo inakuja.
“Kiukweli mwanzo sikupanga kufanya video yake lakini baada ya kuona imekosa airtime ya kutosha kwenye redio nimeshauriwa kufanya video. Kuna watu wengi tayari wameshasema watalipia gharama ya video ya Viva, kwahiyo sasa hivi nipo kwenye maandalizi ya mwisho.”  

-Bongo5 
 
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

No comments:

Post a Comment