Friday 11 September 2015

Video za P-Square hazichezwi na Soundcity TV ya Nigeria toka mwaka 2015 uanze, hii ndio sababu


Kuna kitu kingine nimekifahamu leo baada ya Peter Okoye, mmoja ya mapacha wanaounda Crew ya P Square kuandika kuhusu ishu ni Kituo cha TV cha Sound City kuacha kupiga nyimbo zao !!

Kuna ukweli kwenye hilo, yani TV ya Nigeria iache kupiga Video za mastaa wa nyumbani kwao kabisa ?

Hizi ni #TWEETS nne za Peter wa P Square kuhusu ishu ya TV ya Sound City kutocheza Video zao.Peter P II Peter P
Kwenye majibu yaliyotolewa na Kituo cha TV cha Sound City, wametoa sababu ya kutopiga video za P Square.

Ishu ilianzia December 2014 ambapo TV ya Sound City iliwaalika P Square kwenye event yao, kwenye makubaliano ya kiasi cha pesa ambacho P Square walihitaji kulipwa, Sound City walihitaji majadiliano ili wapate punguzo la bei !! Jibu la Manager wa P Square ambae ni kaka yao mkubwa, Jude ‘Engees’ Okoye hawakulipenda.

Nini mmewahi kukifanya kwa P Square? naomba mniambie hata kitu kimoja mlichowahi kuwafanyia P Square?’- Hii ni nukuu ya alichokojibu Manager wao, Jude Okoye.

Hili jibu halikuwafurahisha, kwa sababu Sound City wamesema wamekuwa na support kubwa sana kwenye Muziki wa P Square toka wakiwa wanaanza muziki, na kuna wakati watu walilalamika kwamba Video za P Square zinapigwa sana mpaka inakera watu wanaoangalia Sound City TV !!


Sound City wamesema kwamba sio hilo tu, kuna wakati P Square walifanya tour ya muziki Africa kwa gharama za TV hiyo… matangazo na kila kitu hawakulipia gharama yoyote, hili la leo kuambiwa hawajafanya chochote haikuwa kitu ambacho walifurahia hata kidogo…

Waliacha kurusha Video za P Square January 2015 na hawana ubaya nao, wanawatakia heri kwenye muziki wao na wako tayari kutoa support ya nguvu kwa kila msanii mchanga ndani ya Africa ili muziki wa kila msanii uendelee kukua.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment