Tuesday 15 September 2015

Shetta: Shikorobo imemtangaza KCEE Tanzania


Muimbaji huyo ameiambia Kikwetu Blog kuwa collabo hiyo haijamsaidia yeye mwenyewe peke yake kwa kukuza jina lake katika nchi za Afrika Magharibi bali pia msanii huyo ameongeza mashabiki katika nchini za Afrika Mashariki.

“KCEE anajihitaji pia kuwa na mashabiki wengine Tanzania na mimi nilihitaji mashabiki kwao. Kwahiyo amenitumia mimi na mimi nimemtumia yeye,” - Shetta.
Video ya Shikorobo haijafanya vizuri nchini peke yake bali pia ilishika chart za vituo mbalimbali vya redio na runinga ikiwemo MTV Base.

Shetta ni mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye Kili Fest Jumamosi ya September 26 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

No comments:

Post a Comment