Tuesday 15 September 2015

Maneno ya Young Dee kuhusu kufananishwa na msanii wa Nigeria, tutegemee collabo kati yao


Akizungumza na ripota wa millardayo.com Young Dee alisema…’Hii ni connection kutokana na sehemu kubwa ya mashabiki wangu walitokea kutufananisha kwa hiyo kadri nilivyokuwa ninaweka picha zangu kwenye instagram ikaonekana mashabiki waki comment na kusema u guys mnafanana sana’ – Young Dee

5 
Msanii wa Nigeria, Patoranking.

Kuna siku niliwahi kumtumia meseji kupitia instagram  akanijibu akasema naye anakutana na hizo SMS kuwa anafanana na mimi, kwa hiyo watu wengi nao walikuwa hawaishii kusema kuwa tunafanana bali kuna watu walikuwa wanasema u guys mnatakiwa mfanye ngoma ya pamoja’ – Young Dee

‘Bahati nzuri mara ya mwisho romy alivyoenda Afrika Kusini alikuwa na show na Diamond akamgusia Patoranking hiyo issue baada ya hapo rommy akanicheki akaniambia kwamba lazima tufanye kitu, sikuamini kwamba labda jamaa ataichukulia serious kwa ukubwa huo baada ya hapo nikapeleka wazo hilo kwenye uongozi kwa hiyo sasa hivi tupo katika mchakato wa kwenda Nigeria kufanya kazi na Patoranking wa Nigeria’ -Young Dee

 


Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment