Tuesday 15 September 2015

Fid Q kurekodi ngoma na rapper K.O wa Afrika Kusini aliyeshirikishwa na Vanessa Mdee


K.O aliyeshirikishwa na Vanessa Mdee kwenye wimbo, Nobody But Me, yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ambako amekuja kujitangaza zaidi kwa mashabiki wa hip hop.

Kwenye ziara hiyo anatembelea vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vituo vya redio na TV.
Akiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM jana Sept 14, mtangazaji wa kipindi hicho Adam Mchomvu alimshawishi rapper huyo kurekodi wimbo na Fid Q.

“Washkajizangu wit ma main man @mrcashtime mr cash time himself kwa fasi za #XXL. Baada ya kumueka @joh_makini kwa @akaworldwide sasa ni zamu ya @realfidq na @mrcashtime … U heeeeaaard,” aliandika Mchomvu kwenye Instagram.

Fid Q atatumbuiza kwenye Kili Festival Jumamosi ya September 26 kwenye viwanja vya Leaders Club.



Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

No comments:

Post a Comment