Wednesday 23 September 2015

Ben Pol kuutumbuiza kwa mara ya kwanza “Ningefanyaje” wimbo mpya aliomshirikisha Avril kwenye KiliFest Jumamosi hii


Ben Pol (2) 

Kwenye wimbo huo uliotayarishwa na producer Mswaki, Ben Pol amewashirikisha Avril wa Kenya pamoja na msanii chipukizi, Rossie M.

Kili Festival itafanyika Jumamosi hii kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na Ben Pol wasanii wengine akiwemo Vanessa Mdee, Weusi, Fid Q, Mapacha Watatu, Ruby, Shettah na wengine watatumbuiza.

Kupitia Instagram, Ben Pol ameandika:

“N.I.N.G.E.F.A.N.Y.A.J.E ambayo inatoka siku ya Alhamisi, 24 September 2015 itakuwa ni wimbo (RASMI) wa pili Kutoka kwa Ben Pol, ikiwa ni baada ya SOPHIA iliyotoka mwezi Januari mwaka huu. Ni miongoni mwa Nyimbo 4 zilizotumika kwenye msimu wa 3 wa Coke studio. Vesheni halisi ya wimbo huu imemshirikisha msanii AVRIL kutoka Kenya pamoja na ROSSIE M kutoka TANZANIA.” - Ben Pol

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

 

No comments:

Post a Comment