Thursday, 27 August 2015

Baada ya kimya kirefu Nemo kuachia ‘Hero’ hivi karibuni


Nemo aliyewahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Number One’ na ‘Wife’ amesema wimbo wake mpya Hero umetayarishwa na Man Walter katika studio za Combination Sounds.

“Kimya kina mshindo niko na mwanangu Man Walter tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha wimbo wangu mpya unaitwa Hero, "amesema." "Nahivi karibuni natarajia kwenda Mombasa kwa ajili ya kufanya video na kuachia ngoma baada ya kurudi."

Nemo amewataka wapenzi wa muziki wa R&B kukaa mkao wa kula kusubiri mziki mzuri kutoka kwake.

-Bongo5

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

 

No comments:

Post a Comment