Thursday, 27 August 2015

AY amewachukua Hermy B na Marco Chali kutengeneza ngoma yake mpya

AY ameshare picha hiyo juu akiwa studio na watayarishaji hao wakubwa nchini wanaowakilisha studio maarufu zaidi, Hermy B wa B’Hits na Marco Chali wa MJ Records.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza AY anakutana tena studio na Hermy B baada ya kuwahi kupishana katika masuala ya kibiashara mwaka 2012.Baada ya hapo AY amekuwa akifanya kazi zaidi na Marco.

“Unategemea kitu kitatokaje?? Best Producers @marcochalitz & @hermyb kwenye chumba kimoja na Mzee wa Commercial.. BIT TINGZ R GWAN!! #ZEE #ElCapo #FAYAAAA #KofiazaMarcoChali,” ameandika AY.

Mashabiki wameonesha kufurahishwa mno na picha hiyo na matarajio yao ni makubwa.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment