Wednesday, 21 June 2017

Hizi ni filamu zilizoingiza pesa ndefu mwaka huu



By: Omary Ramsey

Washapiga hela! Huku mwezi wa sita ukiwa unaelekea mwishoni, tayari makampuni mengi yanayoandaa filamu nchini Marekani yameendelea kujikusanyia pesa za maana kutokana na kuuza muvi zao ambazo nyingi zimeonekana kupendwa mno.

Leo hii! Mtu mzima ninakudondoshea muvi tano ambazo zimepiga pesa ya nguvu tangu mwaka uanze, cha ajabu sasa, nyingine zimetoka hivi karibuni lakini zimekusanya pesa ya kufa mtu. Hapo chini ni muvi hizo tano.

  1. Beauty And The Beast


Hii muvi imetoka tarehe 17 mwezi wa 3 na ndiyo muvi ambayo imetengeneza mkwanja mrefu mpaka sasa hivi. Mpaka leo hii, tayari filamu hii ishatengeneza kiasi cha dola milioni 500.3 ambazo ni sawa na shilingi trilioni 1.6. 

Huu si mwisho, itaendelea kuingiza pesa ndefu kadiri itakavyokuwa ikionyeshwa mara kwa mara.

2. Guardians Of The Galaxy Vol. 2


Hii ni muvi inayoshika nafasi ya pili mara baada ya The Beauty And The Beast kushika nafasi ya kwanza. Hii imezinduliwa tarehe 5 mwezi wa 5 ambapo mpaka sasa hivi tayari ishaingiza kiasi cha dola milioni 375.5 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 700.

3. Wonder Woman



Warner Bros wameleta mapinduzi mengine kama kunogesha vita vyao dhidi ya makampuni mengine ya kutengeneza filamu ikiwemo ya Marvel ambao wanaonekana kama wapinzani wao wakubwa. 

Muvi hii imeshika nafasi ya tatu kwa kuingiza pesa ndefu sana. Imezinduliwa tarehe 2 mwezi wa 6 na mpaka sasa tayari imekwishaingiza kiasi cha dola milioni 279 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 558.

4. Logan



Fox nao hawapo nyuma, wanaonekana kuendeleza mtifuano mzito kuhusiana na masuala ya muvi nchini Marekani. Baada ya kutoa mtiririko wa Filamu za X Men, wameamua kutoa hii ya Logan ambayo wengi wanasema ndiyo filamu ya mwisho kwa Hugh Jackman kuigiza kama Logan. 

Filamu hii ilizinduliwa tarehe 3 mwezi wa 3 na tayari imekwishaingiza kiasi cha dola milioni 226.2 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 450.

5. The Fate Of The Furious



Inawezekana si mategemeo ya watu wengi. Wengi wetu walihisi kwamba filamu hii ingeshika namba moja kutokana na kuwa gumzo duniani. Kampuni ya Universal imekuwa hodari kwa kutoa filamu kali, na hii ni sehemu ya nane ya filamu za Fast And The Furious. 

Ilizinduliwa tarehe 14 mwezi wa 4 na mpaka sasa imekwishaingiza kiasi cha dola milioni 225 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 450.

No comments:

Post a Comment