Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi
watakaochezesha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini
ya umri wa miaka 17 nchini Gabon mwezi ujao.
Mwamuzi msaidizi wa Tanzania, Frank Komba ni kati ya jumla ya waamuzi
29 wa kati na pembeni walioteuliwa katika mashindano hayo
yanayotarajiwa kupamba moto kati ya Mwi 14-28.
Ikumbukwe CAF) haikuteua mwamuzi hata mmoja kutoka Tanzania kwa ajili
ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa
miaka 20 nchini Zambia mwezi uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa na mwamuzi katika fainali za
Afrika kwa vijana kwa miaka mitano iliyopita, jambo ambalo linaanza
kuonyesha huenda kuna baadhi ya waamuzi wameanza kufuata uweledi wa kazi
zao.
Hii ni habari njema kwa soka la Tanzania ambapo wadau wamekuwa
wakipaza sauti zao kutaka wachezaji wa Tanzania kujituma ili kupata
fursa ya kucheza nje lakini pia wamekuwa wakihoji kwa nini makocha wengi
wazawa hawapati nafasi za kufundisha timu nje ya nchi hali kadhalika
kwa waamuzi wa nyumbani wamekuwa hawapati mechi za kutosha za kimataifa
licha ya kuwa na beji za FIFA.
Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ ni miongoni mwa
timu ambazo zitashiriki michuano hiyo ambayo inatarajia kuanza May 14
mwaka huu.
Omaryramsey blog inampongeza Frank John Komba kwa kuteuliwa kuwa
miongoni mwa waamuzi watakaochezesha michuano ya vijana Afrika na
kumtakia kila la heri ili afanye vizuri na kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment