Shemeji wa Kanye West, Khloe Kardashian mwenye ulevi wa kimapenzi na wanamichezo ashindwa kujizuia kwa mcheza kikapu mwingine mkanada.
Ndugu huyo wa Kim Kardashian ‘Khloe Kardashian’ aliyewahi kuwa mke wa mcheza kikapu mstaafu mmarekanai Lamar Odom, amesema kuwa kwa sasa anashindwa kuzuia hisia zake za kimapenzi kwa mcheza kikapu maarufu mkanada Tristan Thompson na kuongeza kuwa anatamani waoane ingawaje mcheza kikapu huyo hajamfuata kwa ombi la mahusiano.
Katika mahojiano na jarida la ES wiki hii, Khole alisema “Ningependa sana niwe na familia,” alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na staa wa kikapu wa NBA … “Actually tumeshazungumzia suala hilo” Alimalizia.
Aliongeza, “Najua ni baba tayari, naamini ni mzazi mwema. Na kutokana na hilo
basi sina shaka yoyote mimi kuwa mama. Lakini sina sababu za kuliangalia
sana hilo. Sio kama mshale wa saa unavyotembea lakini kama katika nasfi
yangu itokee tu” alisema Khloe alipouliza kuhusu kuanzisha familia na
mcheza kikapu Thompson.
Hata hivyo Thompson ana mtoto wa kiume wa miezi minane aliyempata na
mwanamke mwingine jambo ambalo halionekani kabisa kuwa tatizo kwa Khloe Kardashian.
Khloe aliachana rasmi na aliyekuwa mume wake, Lamar Odom Desemba 9,
mwaka jana baada ya ndoa hiyo kuvunjwa mahakamani. Alisifiwa kwa kukaa
kwenye ndoa hiyo kwa muda mrefu kwani aliolewa Septemba 2009 tofauti na
mdogo wake Kim ambaye hushindwa kudumu kwenye ndoa.
No comments:
Post a Comment