Baada ya kuchezea ndoo za jela, hatimae
sasa karudi uraiani. Mkali huyo kutoka Young Money, Rapper Lil Twist
alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kudaiwa kuvunja nyumba ya
muigizaji wa zamani wa Nickelodeon, Chris Massey na kuiba Rolex yake na
kumpiga mwaka 2014.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Twist amethibitisha kwa sasa tayari yupo uraiani. “I’m Home ! Thank God! #YM,”
Akiwa na umri mdogo, rapper huyo alijiunga na Young Money na kuwa na
urafiki na Justin Bieber. Maisha yake yalitawaliwa na kashfa nyingi.
Mwaka 2013, rapper huyo alikamatwa akiendesha akiwa amelewa gari la
Bieber.
Twist ameingia jela Feb. 3 na ameweza kuachiwa huru wiki hii kwa madai yakuonesha tabia nzuri.
No comments:
Post a Comment