Kwa sasa wasanii wamarekani wamekuwa
wakichuana kwa kufanya ziara za kimuziki katika maeneo mbalimbali huku
wengine wakivuka mipaka zaidi mpaka katika bara la Ulaya. Naye Chris
Brown alitangaza ziara yake aliyoipa jina la ‘Party Tour’ ambapo
itawakutanisha mastaa kibao.
Katika ziara hiyo Breezy ilibidi aambatane na wasanii kama 50 Cent, French Montana, Fabolous, O.T. Genasis, Kap G na Casanova.
Bad newz nikwamba Rapper wa nchini
Marekani, 50 Cent amejiondoa kwenye ziara ya ChrisBrown, The Party Tour
katika dakika za mwisho. Amechukua hatua hiyo baada ya kushindwa
kukubaliana kwenye malipo kati ya uongozi wa 50 na promota wa ziara
hiyo.
Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa 50
alikuwa tayari kujiunga kwenye ziara hiyo baada ya mazungumzo ya kwanza
na uongozi wa Chris ambao ulikubaliana kuhusu malipo.
Promota wa Live Nation aliamini kuwa 50
ameridhia na hivyo kumweka kwenye matangazo. Hata hivyo muda wa kusaini
mkataba ulipofika 50 alikuta mpunga ulioandikwa haueleweki na hivyo
kutosa, kwa mujibu wa TMZ.
Kulikuwa na mazungumzo ya kuweka sawa
mambo lakini 50 aliwatolea nje wiki mbili zilizopita. Baadhi ya
mashabiki sasa wamemind wakidai kuwa walinunua tiketi ili kumuona Fiddy.
Kupitia Instagram 50 ameandika: “I would never say my friends can’t afford me. This run wasn’t handled correctly, I’m still on set filming Den of Thieves”.
Ziara hiyo itaendelea kama kawaida leo
huko Baltimore na mashabiki hawatarudishwa fedha zao kwasababu Chris
atakuwepo kama kawaida.
No comments:
Post a Comment