Tuesday 28 March 2017

Dayna Nyange alia ‘njaa’ kwenye muziki


Mwanamuziki wa kike anayefanya poa Bongo na Wimbo wa Komela, Mwanaisha Saidi ‘Dayna Nyange’ amefunguka kuwa kwa sasa mambo yamekuwa magumu kwenye Tasnia ya Muziki Bongo kiasi kwamba shoo zimekuwa adimu kupatikana jambo linalosababisha njaa kwa wasanii wengi.

 Akipiga stori na Showbiz, Dayna alisema kwa sasa mambo si kama miaka ya nyuma ambapo wasanii walikuwa wanakaa na kuwasubiri mapromota ili wawape shoo, kwa sasa  wasanii wanatakiwa kutengeneza mipango ya kuandaa shoo wao wenyewe au kwa kuwatumia mapromota wachache waliyopo kwenye gemu.

 “Kwenye muziki mambo yamekuwa taiti si kama zamani, na si kwenye muziki wetu tu wa Bongo Fleva mimi nazungumza na watu wanaofanya mpaka Muziki wa Dansi, nao wanalia njaa hivyohivyo, mifukoni hakuna kitu na ili kupata chochote mtu inabidi kupambana kwelikweli kutafuta namna ya kupiga shoo na kutotegemea muziki pekee,” alisema Dayna.

No comments:

Post a Comment