Baraza la Sanaa Taifa ‘BASATA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’
wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa
kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili
kutokana na wimbo huyo.
Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna
maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea
kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.
Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza
kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika
kuwa na kosa la jinai.
“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji
msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,”
Basata walitweet.
Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye
taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati
cha polisi.Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika
vyombo vya habari. Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha
taratibu za kipolisi,”
Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.
No comments:
Post a Comment