Wednesday, 21 October 2015

Uliokuwa uongozi wa Young Dee watoa ofa ya video moja kwa kundi alilojitoa la Mtu Chee


Kundi la Mtu Chee lililoanzishwa na rappers Stamina, Country Boy na Young Dee, leo wameachia single mpya bila Young Dee huku wakiwa wamemwongeza Young Killer kwenye single hiyo.

Young Dee alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa uongozi wake (MDB) ulimzuia kuendelea kuwa member wa kundi hilo.

Millian amethibitisha kutohusika katika maamuzi ya Young Dee kujiondoa Mtu Chee, kwa kujitolea kuwapa ofa ya video ya wimbo mmoja kundi hilo.

Kupitia post ya Instagram ya Country Boy, Millian alicomment kwa kuandika;
“Natoa offa ya kuwafanyia music video yenu moja bure wanangu. Dee farasi sana alivyosema Eti management yake imemzuia kufanya Kazi Na nyie @countryboytz @youngkillermsodoki @staminashorwebwenzi”

Country boy alijibu;
“thanx bro tunapokea na tunajua umuhimu wako kaka mkubwa Asante tupo tayari” 



maxi na mtu chee 
Ingia hapa ku-download hii ngoma yao mpya Mtu Chee - Mtu Tatu

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

 


No comments:

Post a Comment