Monday, 12 October 2015

Diamond: Tuzo za AFRIMMA ni kwa ajili ya Tiffah

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alipata tuzo tatu za AFRIMMA nchini Marekani amesema kuwa tuzo hizo ni maalum kwa mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni,Tiffah.

Akipiga stori na B Dozen ambaye alikuwa kwenye tuzo hizo alisema kuwa ilikuwa ni moja ya ndoto zake kuwa akipata tuzo huku akiwa amepata mtoto itakuwa maalum kwa ajili ya mtoto wake.

‘’Unajua ilikuwa ni moja ya ndoto zangu kuwa yaani siku nimepata tuzo halafu nina mtoto naidedicate kwa mwanangu inaleta picha nzuri sana tangu niwe na mtoto najitahidi kufanya kazi kwa umakini sana natamani mwanangu akue anikute Diamond wa leo awe ni Yule Yule,’’alisema Diamond.

‘’Mwanagu amekuwa akinipa changamoto nifanye kazi sana,nafikiria sana kama kutunga nitunge sana kama kujituma nijitume sana kwa kila nitachokifanya huwa namuwaza kwenye kichwa changu ndiyo maan nikasema hii tuzo ni maalum kwake,’’aliongeza Diamond.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment