“Kiukweli
mimi kama artist nipo dilemma, kwa sababu kwa utaratibu kama msanii
akiachia nyimbo anasambaza katika radio station, unapopeleka nyimbo yako
katika vituo vya redio baadaye utataka feed back ngoma yako
imepokelewaje, imepita na inachezwa na watu wameipokeaje? Kwahiyo baada
ya Roma kufanya hilo zoezi si kila media ilipokea nyimbo na ikaipiga.
Kila redio ilikuja na jibu lake tofauti kwamba, hii nyimbo hapana
hatujaruhusiwa kama kituo cha redio kuipiga. Wengine wakasema
tunaicheza lakini hatutaicheza tena kwa sababu ina maneno fulani hivi
makali sana,” - Roma.
“Na
wengine wengi wanaipiga mpaka sasa hivi na imeshaingia kwenye chati
mbalimbali za redio. Lakini lile tamko rasmi kwamba nyimbo imefungiwa
mimi sijapata kutoka kwenye mamlaka fulani husika zaidi baadhi ya redio
zinasema nyimbo yako imefungiwa, ukienda kwingine sisi tunaicheza,”
aliongeza Roma.
Kwa upande mwingine Roma amesema video ya wimbo huo inakuja.
“Kiukweli
mwanzo sikupanga kufanya video yake lakini baada ya kuona imekosa
airtime ya kutosha kwenye redio nimeshauriwa kufanya video. Kuna watu
wengi tayari wameshasema watalipia gharama ya video ya Viva, kwahiyo
sasa hivi nipo kwenye maandalizi ya mwisho.”
-Bongo5
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment