Monday 21 September 2015

Izzo Bizness awashirikisha Mwana FA na G-Nako katika ngoma yake mpya 'Shem lake'


Izzo ameiambia Story Tatu ya Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa anajisikia faraja kufanya kazi na rapper kama FA ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki wake kwa nyakati tofauti.


"Ngoma yangu mpya nimewashirikisha G-Nako pamoja na Mwana FA na producer aliyetengeneza beat ni Nahreel kutoka The Industry," - Izzo Bizness

Hii itakuwa project tofauti kwa sababu ni ngoma yangu ya kwanza kufanya kazi na Mwana FA, najua FA ni rapper mkubwa, rapper ninayemuheshimu sana, rapper mwenye uwezo wa hali ya juu. Pia G-Nako ni chorus killer ambao tunao Tanzania, kwa hiyo mashabiki wasubirie kitu kizuri kinakuja," aliongeza Izzo Bizness

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment