Tabia ya watu kutumia majina ya wasanii kwenye mitandao na kujifanya wao ndio wasanii wenyewe na kukutana na wale wasio jua kuhusiana na mambo ya kwenye mitandao kisha kuwalaghai na kuwataka pesa sio hapa Bongo tu bali hata nje ya Bongo tabia hizo zipo.
Nchini Kenya imemkuta dada huyu anayeitwa Priscah ambaye kwa sasa yupo Lebanon kwa kazi zake ambapo alikutana na account feki inayotumia jina la Shetta Shetta Shikorobo. Dada huyo baada ya kutumiwa friend request na account hiyo akawa ni rahisi kuwaamini haswa pale walipoanza kuchat naye hadi kufikia kumuomba pesa.
Pia ushawishi wao haukuwa wa hivi hivi bali wakamshirikisha na Diamond Platnumz kwakumzushia kuchukua gari la Shetta baada ya ngoma ya Kerewa. Jamaa hawa walilalamika kutokuwa na fedha lakini baada ya kutumiwa ya kwanza wakahitaji ya pili na ndipo wakaanza kumgeuka dada huyu hadi kufikia ku m block.
Usiku wa kuamkia leo baada ya kutumiwa voice note na dada huyu nikaamua kumtafuta Shetta ambaye yupo Afrika Kusini ndipo alipo nijibu kwa uwazi kuwa hana account yoyote ya facebook mbali na Facebook Fan page.
Usiku wa kuamkia leo baada ya kutumiwa voice note na dada huyu nikaamua kumtafuta Shetta ambaye yupo Afrika Kusini ndipo alipo nijibu kwa uwazi kuwa hana account yoyote ya facebook mbali na Facebook Fan page.
Hizi ni picha za chat ya dada huyo wakati akilaghaiwa hadi alipoona wanaanza kumpotezea.
Share na wenzako ili wasitapeliwe kama huyu.
-Tubongetz
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment