Wednesday, 12 August 2015

Audio | Ben Pol asema Mr Blue amewainspire wasanii wengi sana yeye akiwa mmoja wapo

Ben Pol amesema Mr Blue ni msanii aliyewavutia wasanii wengi kufanya muziki akiwemo yeye mwenyewe.
Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Ben Pol amesema kipindi Mr Blue anatoka, aliweza kuwapa ujasiri vijana wengi wenye umri mdogi kufanya muziki.

“Kiukweli mimi huwa nawaambia hata wasanii wengine wa age yangu ‘unajua ninyi Byser katuinspire watu wengi sana tutake tusitake.’ Kwasababu kwa age yake halafu akatoka kila mtu akawa anasema ‘dah I wish niwe kama Byser,” amesema Ben.

Anadai kuwa wasanii ambao kwa sasa wana umri wa kuanzia miaka 24 – 26 wengi walimuona Blue kama msanii wa mfano.

Ben Pol alidai aliimba wimbo wa Mr Blue kwenye usaili wa kuingia THT.

Sikiliza kipindi hicho hapo chini.



-BONGO5

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

No comments:

Post a Comment