Friday, 29 May 2015

Ulimmiss Mke Wa Marlaw,Besta Arejea Studio Round Hii Anafanya Album Mpya Baada Ya Kupata Mtoto Wa Pili.



“Narejea kwenye muziki kwa nguvu zote.” Hiyo ni kauli ya msanii wa kike Besta, ambaye alisumbua na video ya wimbo wake wa ‘Baby Boy’ miaka kadhaa iliyopita, kabla ya ku-fall in love na muimbaji wa ‘Pii pii’ Marima Lawrence a.k.a Marlaw ambaye sasa ni mume wake.
Baada ya kujifungua mtoto wa pili wa kiume mwaka huu, Besta Prosper Rugeiyamu anayefahamika zaidi kwa jina moja Besta, ameiambia Bongo 5 exclusively kuwa sasa yuko tayari kurudi kwenye muziki na anakaribia kukamilisha album yake mpya.

“Kuna project nafanya kwahiyo ni album, kuna nyimbo ambazo nilizirekodi wakati bado sijajifungua na nyingine ndo nazimalizia nyimbo tatu za mwisho halafu ndo naanza kutoa, kwahiyo zimebaki nyimbo mbili. Itakuwa na nyimbo kumi na tano, kwahiyo kama nitazipunguza kidogo au kutoa zote sawa.” Alisema Besta a.k.a Mrs Marima.
Besta amepost picha hii Instagram na kuandika:#MamaRences#BackToBusinessPreparation

Besta ambaye August 2013 alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kiume, amesema anazo sababu za kuamua kufanya album licha ya changamoto za soko la album za muziki Tanzania.

“Cha kwanza mi napenda kutoa album hata kama maslahi yamepungua kuna matatizo kwenye mambo ya album, lakini bado najua mashabiki wanahitaji kupata album, waone kazi sio kazi moja moja, na kwa upande wa kutoa hizo nyimbo nitaangalia kwasababu of course nafanya muziki na pia tunataka tutengeneze hela, kwahiyo ntatafuta njia nzuri ambayo itanifanya nitengeneze hela kupitia hizo nyimbo kwasababu kuna mambo mengi kuna ringtone kuna vitu vingi.”

Maproducer waliohusika kutengeneza album hiyo ni pamoja na Fundi Samweli pamoja na producer wa Uganda aliyekuwa akifanya nyimbo za Besta miaka ya nyuma.

“Studio nimefanya na sasa hivi kuna technology kwahiyo nimefanya na maproducer mbalimbali ambao wako nje, nimefanya pia na Fundi Saweli nyimbo nyingi na producer wangu wa Uganda.”

Kuhusu wasanii ambao amewashirikisha kwenye album hiyo amesema wapo lakini ni surprise.

Besta amesema kuwa mashabiki wajiandae kupokea wimbo wake wa kwanza miezi miwili kuanzia sasa, lakini video itachelewa kwa miezi mitano.

“Yaani haizidi miezi miwili wataanza kusikia wimbo ya kwanza, lakini video itachelewa kidogo kwasababu niko kwenye mazoezi, itakuwa baada ya miezi mitano hivi, lakini wimbo wa kwanza haitafika August utasikika.”

FOLLOW US ON

No comments:

Post a Comment