Biography Ya Sammisago
Misago Samuel Kasago Aka Sammisago Jina nalotumia kwenye radio, tv na mitandao ya kijamii nilizaliwa Dar es salaam 6 Feb 1986 kwa wazazi wangu nikiwa mtoto wa pili baada ya Kaka yangu Isreal na anayenifuatia ni mdogo wangu wa kike Gift.
Shule
Sammisago amesoma Shule ya msingi Arusha School iliyoko jijini Arusha, secondari nimesoma kidato cha kwanza Arusha Meru na kumalizi Kidato cha pili mpaka cha nne Uganda [Kabojja International School] iliyopo Natete.
Baada ya kidato cha nne nilisoma Certificate ya Information Technology mwaka mmoja, Certificate ya Education miaka miwili kwenye chuo cha St Mary’s na Degree ya Business Administration kwenye chuo cha LearnIt Dar es salaam.
Radio
Wakati nasomea IT nilipewa nafasi ya kuwa mtangazaji kwenye kituo cha radio cha Tripple A Arusha na Radio Manager wake wakati huo alikuwa Sophia Kessy nakupewa vipindi vitatu kikiwemo cha Drive [4:00 to 6:00 ], kipindi cha filamu na kipindi cha Weekend Vibe cha jumamosi, nilifanya kazi kwa miezi minne.
Mwaka 2008 mpaka June 2009 nilikuwa nikisomea Education huku nikifanya kazi Magic Fm kituo cha radio cha Africa Media Group, Nafasi niliyopewa na Dativas Mango [Gomba Gomba ] radio manager wa Magic Fm wakati huo.
Marafiki kama Nick Ngonyani, Tahjir Siu, Salma Msangi, Mish B, Allen Kasiga nawapa shukrani sana.
Marafiki wengi walikuwa wakinishawishi niwe mtangazaji wa tv huku wakiamini ni kazi niliyoumbwa kufanya, washkaji kama [Babu wa kitaa, Langa, Adam Mchomvu, Izzo Bizness na B Dozen ] walihusika sana kunishawishi kuwa bora kila siku.
Radio Na Tv
4 August 2009 nilipewa nafasinyingine kubwa ya kujiunga na East Africa Radio na Tv kama radio presenter wa kipindi cha Power Jams, baada ya mwezi nikapewa nafasi ya kuendesha vipindi vingine viwili [ Top 20 na Satuarday Hot Mix ]. Kabla ya mwaka kupita uwezo na juhudi zikafanikisha nafasi nyingine ya kuendesha kipindi cha tv cha Friday Nite Live.
Sammisago.com ni mtandao nilioanzisha kama sehemu ya kushare mambo nayofanya na watu wangu,mtandao ambao baadae umekuja kuwa sehemu kubwa ya maisha yangu huku kila habari nayopata inapatikana hapo.
Shukrani kubwa kwa MD wa Eatv Regina Mengi, HP Lidya Ibaraguza na HP Wa Earadio Nasser Kingu.
Music
Vitu vingi napenda kufanya kama Rap na kuigiza ila nakosa muda wa kutoa kazi baada ya kurekodi. Nimewahi kurekodi na producer G Son na Nahreel Tu.
Miaka kadha nyuma ya Mic imewezeshwa na Mwenyezi Mungu Tu, Ukimwamini, kumshukuru na kumuomba yote yatawezekana.
Sammisago.
No comments:
Post a Comment