Friday 29 May 2015

Basi ishu ya Miss TZ ikaingia kwenye mjadala wa Bungeni Dodoma, kumbe kuna Wabunge hawaitaki ??


Kwenye maswali na majibu ndani ya Kikao cha Bunge kibachoendelea Dodoma kuna vingi vinatokea, sasa hivi ni mijadala ya Bunge la Bajeti lakini ikifika wakati wa maswali na majibu kuna ishu nyingine huwa zinaibuliwa humohumo.. Leo niliinasa hii ya mashindano ya Miss Tanzania, kumbe kuna Wabunge hata hawayataki mashindano hayo kabisa !!
Mimi sioni haja ya mashindano ya mamiss Tanzania.. Sisi tunaongozwa na maadili, unamuona mtoto wako anaenda kushindana mamiss, na ipo Kitaifa kabisa Mheshimiwa Fenela? Unamuona mtoto anavyodhalilishwa kwa sababu ya gari.. Jamani kama hamna gari bora mpande baiskeli au mpande pikipiki majumbani mwenu“>>>Mbunge Faida Mohamed Bakari.

Sisi wazazi hasa wanawake hatutaki.. Serikali inashadadia umiss hasa mimi nasema huu umiss una faida gani katika nchi yetu? Mbona hawafanyi na wanaume?“>>> Faida Mohamed Bakari.

Pamoja na yale mapungufu ambayo ameyagusia miss Tanzania ni suala la kisanii na yale mapungufu yalifanyiwa kazi na tukaruhusu Miss Tanzania ikaendelea“>>> Fenela Mukangala.

Ikafika time ya maswali kujibiwa >>> “Miss Tanzania inatengeneza ajira kwa warembo na pia inatangaza nchi na vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi na pia inatoa burudani na elimu. Tunao warembo wenye akili nzuri wanaotumia nafasi ya Miss Tanzania kutengeneza ajira kwa vijana wengine“>>> Waziri Fenela Mukangala.

 Iko hapa sauti, ukiplay utasikiliza swali la Mbunge huyo na jibu la Waziri ilivyokuwa Bunggeni Dodoma.


credit : millardayo

FOLLOW US ON

No comments:

Post a Comment