Wednesday 8 April 2015

Joslin na Mr Blue hawaelewani? Ruby anatamani wimbo wa Vee Money?.. Shamsa Ford, Nay… #255



Huenda na wewe uliwahi kusikia kuwa msanii Joslin na Mr Blue hawaelewani.. 255 ikaanza kwa kumtafuta Joslin ambae amesema hawajawahi kuwa na tofauti ila kwa sababu walitoka wote kwa wakati mmoja na wote wakawa wanafanya vizuri watu wakazusha story ya namna hiyo.

Joslin amesema mara nyingi walishafikiria kufanya collabo lakini majukumu yamefanya kuwe na ugumu hilo kutimia, lakini anaamini kuwa ikitokea wakakutana studio lazima wafanye collabo.

IMG_0023Ruby ndio jina jingine la msanii wa kike ambaye yuko juu kwa sasa.. Ruby amesema ikitokea akaambiwa arudie wimbo wa msanii yoyote wa hapa TZ, atachagua kurudia wimbo wa ‘Closer’  wa Vanessa Mdee kwa sababu  anampenda na anaupenda wimbo huo.
sm nJana jioni mitandao ilikuwa na story nyingi.. yote yalitokana na picha iliyosambaa ikimuonesha muigizaji Shamsa Ford akipigana busu na msanii Nay Wa Mitego, watu wakahisi moja kwa moja kwamba wana uhusiano wa kimapenzi, ni kweli?
Shamsa ana jibu hili.. Hizo picha ni za movie mpya inayoitwa ‘Manyaunyau’ ambayo iko kwenye hatua za mwisho, picha hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya promo ya movie hiyo lakini hawana uhusiano wowote.. wao ni marafiki na wanaheshimiana.
Shamsa amesema kaachana na mume wake toka mwaka jana, ila kwa sasa yuko karibu na Nay kwa mambo ya kazi.
Bonyeza play kusikiliza story zote za 255 ya leo…


No comments:

Post a Comment