Saturday 17 January 2015

Diamond aeleza Kuhusu Collabo yake na P-Square

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye huwa hafanyi makosa pale anapopata nafasi wa kukutana na fursa zinazoweza kumvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine katika muziki wake hivi karibuni nchini Nigeria alipata nafasi ya kukutana na wasanii wakubwa wa nchini humo na kubadilishana mawazo.

Nyota huyo anayetamba na wimbo wa ‘Nitampata Wapi’ alipokuwa Nigeria alikutana na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo P-Square, Fally Ipupa, Flavour na wengine ambapo kwa kanuni yake Diamond anadai huwa hafanyi makosa anapopata nafasi kama hizo, Je tutapata nafasi ya collaboo na P-Square?.

“Mimi kanuni yangu kama ilivyo, nikikutana na 18 huwa siachi yaani naachia bonge la shuti mpaka nishinde kwahiyo vitu vyote vimekaa vizuri, lakini sio vizuri kuongea sana kwasababu vitu vingine bado viko chini ya kapeti…so watu wategemee vitu vizuri najitahidi sana kwenda resi na speed zote pale napofikia mimi niweze kufanya kitu kiwe kizuri.” Amesema Diamond

Kutokana na kauli hiyo mashabiki wa Diamond watarajie chochote kikubwa kutoka kwake kwani amethibitisha kuwa kila kitu kiko vizuri na kwa sasa anataka kwenda kwa kasi kidogo ili aende na muda.

Aidha, Diamond ameachia wimbo mpya wa miondoko ya mduara unaoitwa ‘Nasema Nawee’ ambao inasemekana kuwa umevuja japo haijadhibitishwa na muhusika.


Source : Times Fm

FOLLOW US ON


No comments:

Post a Comment