Saturday, 29 November 2014

Snura Aangua KiLIO Mara Baada Ya Kusikia Ngoma Mpya Ya Kala Jeremiah

na hiki ndicho alichokiongea snura mushi.. Dah!! Maisha haya bwana hayaeleweki kama unga wangano chapati, maandazi, mikate, sambusa, visheti, kalimati, uji, mpaka gundi yakubandikia matangazo mitaani.....

Hivi inakuaje mtu unakataa mimba yako au mtoto wako...wakati unafanya ulikua unasikia rahaa maneno yote unamaliza ..inamaana ulikua hujui unachokitoa kinakwenda kutengeneza nn au mnawaonea wanawake kwasababu mtoto hukaa na kujitengeneza kwenye matumbo yao...hivi mnajua miezi tisa ya kumbeba mtu kwenye tumbo mpaka kumzaa mwanamke anapata uchungu gani mpaka naww umuongezee wa kwako...acheni hizo bwana nyie wanaume wenye tabia hizo....kama unajiona ww hutaki mtoto au unaogopa majukumu condom zimemwagwa kama pipi madukani.....usijitie mapana ya pazia la sinema mwisho wa siku hata kununua udongo wa mia huwezi....au utasikia wanasema....kataka mwenyewe.....nyoooo kataka mwenyewe ulisikia wapi mtu kaukorogea uji akaupa unywe hicho ndio chakula chake nayy anahisia kama ulizokua nazo ww nandio maana ulivyotema sumu zako akakuelewa kama mmependana na raha mkapeana bas likitokea mnashirikiana au siku hizi kuna wanawake wanabaka? na kama humpend ungemuacha ulimfatia nn na unaowapenda wapo....maana wengine wakishatia mimba utawasikia yule sio chaguo langu ....

Sio chaguo lako wakati ushaharibu KWALEO NGOJA NIISHIE HAPA poleni wanawake wenzangu ambao yamewakuta haya Mungu atawakuzia watoto wenu na watakua imara @kalajeremiah umenifanya nimeandika kwa hasira huyo dada anaelia kwenye video amenifanya mpaka nimehisi kweli.....napenda sana watoto.....pia nawapongeza wanawake majasiri mnaoanguka na kuinuka na watoto wenu wenyewe bila msaada wa baba...na nnawapa hongera wanaume wote mnaowatunza watoto wenu Mungu awabariki sana..........kama nimekukwaza basi unahusika...pole na ikiwezekana badilika........# watoto ndio taifa la kesho 


FOLLOW US ON


No comments:

Post a Comment