
Baada ya Diamond kuachia video ya ‘Ntampata wapi’ iliyofanyika Afrika Kusini, amekutana tena na maswali aliyokutana nayo kipindi alipoachia video ya ‘Mdogo mdogo’, ya kwanini amewatumia zaidi wazungu kwenye video ya wimbo wake wenye ladha ya Kiafrika.
Hili ndio jibu la Platnumz baada ya
kuulizwa swali hilo kwenye kipindi cha Power Jamz kupitia East Africa
Radio: “Kuna kitu kimoja, waache ubaguzi inategemea na script ya nyimbo
inavyozungumza, script inataka kitu gani, script yangu ya mdogo mdogo
ilikuwa inazungumza kwamba mapenzi hayachagui, ndio maana kulikuwa na
familia ya kizungu mimi familia ya kiafrika, mimi namtaka demu wa
kizungu lakini wazazi wake hawataki, kwahiyo ndo maana mwisho tukaandika
mapenzi hayachagui”.
“Na naamini hicho kitu ndo
kilisababisha kufanya hata Marekani ikashinda tuzo, video ya Aye
haikushinda ikashinda video ya Mdogo mdogo kama video ya Afrika
kwasbaabu concept yenyewe ilikuwa inazungumza vizuri, wazungu wenyewe
wameona kama aah hii kweli lakini tuache maswala ya kibaguzi”.
No comments:
Post a Comment