Hatimaye kundi la”Wakali sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo lilikuwa miongongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linaloratibiwa na Kituo cha East Africa Television ltd na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, limeibuka mshindi katika shindano hilo lililokuwa la kukata kwa shoka kwa ushindani mkali katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makundi matatu yaliyofanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika
hatua ya fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri
mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi
walioibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone ikiwa na muda wa maongezi wa sh. 100,000.
Mshindi wa pili ni kundi la The W.T. na kuondoka na kitita cha shilingi
Milioni 1 na laki 5 na mshindi wa tatu ni kundi la Wazawa Crew na
kujinyakulia shilingi laki 5.
Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la
jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano
wa fainali wa shindano hilo lililoandaliwa na EATV lililofanyika
kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,ambapo kundi
la”WAKALI SISI” liliibuka washindi na kunyakua kitita cha shilingi
Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Kundi la”Wakali sisi”ambao ni mabingwa wa shindano la Dance 100%
2014,wakionesha umahiri wao wa kucheza wakati wa fainali ya shindano
hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco
Oysterbay jijini Dar es Salaam na kuweza kujinyakulia kitita cha Tsh
Milioni 5 toka kwa mdhamini mkuu wa shindano hilo Vodacom Tanzania.
Kikundi cha The WT cha jijini Dar es Salaam kilichoshinda nafasi ya pili
katika fainali ya shindano la Dance 100% 2014 likionesha umahiri wao wa
kudansi katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.Ambapo kundi
la”WAKALI SISI”toka kiwalani jijini liliibuka na ushindi huo na
kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa
shindano hilo Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia)
akitaniana na kiongozi wa kundi la”Wakali sisi”la kiwalani jijini Dar es
Salaam,Baraka Kambona(kushoto)alipokuwa akikabidhi hundi yenye thamani
ya Tsh Milioni 5 kwa kundi hilo kama wadhamini wakuu wa shindano la
Dance 100% kundi hilo liliibuka washindi katika fainali ya shindano
hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki Don Bosco Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Washindi wa shindano la Dance 100% 2014 kundi la wakali sisi wakiwa kwenye picha ya pamoja na majaji wa shindano hilo na Ofisa matukio
wa Basata Kurwijira Magesa (kushoto)pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili toka kulia) mara baada ya
kutangazwa washindi wa shindano hilo na kujinyakulia kombe pamoja na
kitita cha shilingi milioni 5 toka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo
Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment