Kama asingekuwa rapper, Young Killer Msodoki angekuwa shehe anayeswalisha msikiti au mcheza kabumbu.
Young Killer akiwa na mpenzi wake Halima pamoja na rafiki yao.
Young Killer amesema muziki kwake umekuja tu na sio kitu alichotegemea kufanya.
“Kiukweli kabisa mimi nilikuwa najua nakuja kuwa mchezaji na sio
msanii,” rapper huyo ameiambia Bongo5. “Nisingekuwa shehe, ningekuwa
nchezaji. Yaani shehe, mchezaji au msanii, ila sana sana usanii ilikuwa
haipo. Nilikuwa nilikuwa ni mtu ambaye narap home home si unajua zile!
Lakini vitu ambavyo nilikuwa nimevishikilia sana na nilikuwa naamini
vitakuja kunitoa ni kuwa shehe au kuwa mchezaji mpira,” ameongeza
Msodoki.
Pia Msodoki ambaye ni shabiki wa timu ya Yanga amefunguka ya moyoni juu ya machungu ya timu yake inapoteza mchezo.
“Kuanza kuishabikia timu ya Yanga nimeanza nikiwa na kama miaka 10
fUlani hivi. Yanga ni timu yangu kitambo na inapofungwa naumia sana hasa
tukifungwa na Simba hiyo siku kwangu itakuwa mbaya na nitalala mapema
sana kwa sababu nakosa raha kabisa.”
No comments:
Post a Comment