Rapper kutoka Rock City, Young killer Msodoki wiki hii amerekodi wimbo mpya ambao amemshirikisha kaka yake rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, ambaye pia anatoka Mwanza.
Msodoki amezungumza na Bongo 5 kuhusu wimbo huo, “Ni project mpya kabisa kali naweza kusema kwasababu imekutanisha wakali wawili halafu kutoka mji mmoja”, alisema Killer.
Amesema kuwa jina la wimbo huo ’13’, limetokana na tarehe ya kuzaliwa yeye na Fid ambao wanashare tarehe moja ya kuzaliwa lakini mwezi na mwaka tofauti.
“Hii ngoma inaitwa ‘Kumi na Tatu’ (13), kumi na tatu ni tarehe ila hatujaamua kuiita tarehe 13 ila inaitwa 13, kwasababu tarehe 13 ni siku ambayo kazaliwa Fid Q na ndio siku ambayo nimezaliwa mimi kwahiyo wote ni 13, kwahiyo ngoma tumeamua tuiite 13.” Fid amezaliwa August 13 huku Msodoki April 13.
Ameendelea kusema kuwa ‘Kumi na Tatu’ imefanywa na maproducer wanne akiwemo mkongwe P-Funk Majani.
“Ni ngoma ambayo imefanyika Bongo Records producer akiwa ni Majani, ila beats wakiwa wamepiga watu tofauti tofauti, kuna Lollipop, kuna Amiga Tyga, kuna Palla Midundo. Hawa ni watu watatu ambao kila producer nilikuwa nikimpelekea namwambia afanye kitu kimoja ambacho yeye anaweza akafanya…ndio nikafanya kitu kimoja ambacho ambayo vocal ndio akafanya Majani”.
Young Killer alishare picha IG wakiwa studio na kuandika:
“#ILIKUWA SIKU YA FURAHA SANA JANA BAADA YA KUKAMILISHA NDOTO YANGU YA KUFANYA KAZI NA (p.funky MAJANI) ha ha ha
RAHA SANA @majani187 (13) kumi na tatu ). Ha ha ha imenipa wakati mzuri xana wa kutabasamu.. Ha ha ha ha”
RAHA SANA @majani187 (13) kumi na tatu ). Ha ha ha imenipa wakati mzuri xana wa kutabasamu.. Ha ha ha ha”
Mashabiki wa Msodoki wakae mkao wa kula sababu collabo hiyo inatarajiwa kutoka siku si nyingi.
“Kutoka nadhani inaweza ikawa kama wiki moja na nusu mbele itakuwa imetoka kwasababu hapa video ya ‘Umebadilika’ muda si mrefu nitai release, kwahiyo nitaipa gap kidogo kama wiki moja na nusu wiki mbili flani ntai release ngoma”.
No comments:
Post a Comment