Sunday, 28 September 2014

‘Nammiss sana Mangwair’, asema TID, walikuwa waanzishe kipindi cha TV

Mwanmziki wa BongoFlava TID anasema anammiss kupita kiasi swahiba wake, marehemu Albert Mangwea aka Ngwair.

T I D amesema Ngwair alikuwa na msaada mkubwa kwenye muziki wake.

“Unajua kukosekana kwa Ngwair kwangu ni pengo ambalo siwezi kulisahau kabisa,” amesema muimbaji huyo. “Unajua ua Ngwair kuna ngoma tulikuwa tunafanya wote na msaada wake nilikuwa nauhitaji sana maana touch zake zilikuwa nzito. Kama nyimbo zangu ‘Kiuno’,’Raha’,’Check Me’, zote hizo ameandika yeye Ngwair. Ukiacha hizo tulikuwa tunataka kuja na kipindi cha TV, kufanya movie ya Girlfriend Part 2. Vitu vyote hivyo ni mtu ambaye tulikuwa tumeanza naye. Leo unaona hayupo najiona nipo mpweke sana, maana ni mtu ambaye alikuwa akinipa idea, aisee nammiss sana,” ameongeza TID.

Kwa upande mwingine TID amezungumzia uhusiano wake na Dully kutokana na taarifa za hivi karibuni kuwa walizinguana.

“Mimi na Dully hatuna tofauti tu ni chalenji tu na juzi Dully alikuja home tuakenda studio tumerekodi ngoma ya pamoja. Kwahiyo sisi tunafanya chalenji ili tufanye kitu kizuri. Dully ni kama brother wangu amenipita mimi kama mwaka mmoja na mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanza kumtambulisha Dully stejin pale Bills enzi hizo miye nilikuwa MC wa hapo.”

JOIN US 

FACEBOOK/ OMARYRAMSEY

TWITTER/ @RAMSEYOMARY

 

No comments:

Post a Comment