Director Adam Juma wa kampuni ya Visual lab/Next Level, amempongeza rapper wa Mbeya Izzo Bizness na director wake Nick Dizzo kwa kutaja gharama halisi waliyotumia kushoot video ya ‘Walala hoi’ambayo Izzo amesema ni shilingi milioni 1 na laki 4 tu. “Video ni milioni 1 na laki 4 na Nick hapo tumemlipa kila kitu”
Akizungumza na Enewz ya EATV, Izzo amesema video imechelewa kukamalika kwa sababu muongozaji wake amekuwa na kazi zingine nyingi wakati huu.
“Kuna vipande vichache tu vimebaki kwa sababu nyimbo yenyewe unaiona ilivyo, tumeongea mambo mengi, na sio muda ambao unahitaji kushoot unashoot tu. Unaweza ukahitaji kushoot director ana kazi nyingine tatu, nne kwahiyo unasogezwa mbele. Ndio maana imechelewa. Pia watu wategemee video kali kabisa. Video ni milioni 1 na laki 4 na Nick hapo tumemlipa kila kitu,” alisema Izzo.
No comments:
Post a Comment