Thursday, 21 August 2014

Haya ndo Maajabu ya Nguo za Mitumba



NGUO ZA MITUMBA NI HATARI SANA, HEBU SOMA HAPA CHINI
hao unaowaona kama weusi weusi kwenye ziwa hapo ni funza ambao wameform matobo matobo ambapo wanatoka nje sasa baada ya kukomaa ki ukweli tunatakiwa tuwe makini sana na nguo hizi za mitumba tunatakiwa tuzifue kwa maji ya moto ili kuua vimelea na madawa yaliyopuliziwa vinginevyo tutaumia sana na hii pia ni fundisho kwa wale wenye kuvaa nguo za ndani za mitumba pia bila kuzifua wadada na wakaka tuweni makini kwenye mavazi yetu ukiona ujumbe huu mtaarifu na mwenzio auone SHARE,LIKE and COMENT kwa manufaa ya wengine


Pia Daktari wa magonjwa ya ngozi, Anngie Krogh anasema kuna madhara makubwa yanaweza kuwapata watumiaji wa nguo hizo hasa kutokana na maeneo hayo yanayovaliwa kuwa na unyevu nyevu mara zote.
“Pamoja na kutakiwa kufuliwa, kuanikwa juani na hata kupiga pasi, bado nguo hizo zinahitaji zifuliwe kwa kutumia sabuni ya dawa yoyote ya kuua vijidudu, yapo magonjwa mengi ya ngozi ya kuambukizwa ndiyo maana mara zote tuna shauri kuepuka kuvaliana nguo,” anasema.
Anasema zipo takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wengi ndio wanaofika katika hospitali za magonjwa ya ngozi kuhitaji huduma za matibabu na hiyo inasababishwa na maumbile ya wanawake ambayo ni rahisi kuambukizwa tofauti na wanaume.
Anatolea mfano vijidudu vya fangasi vimekuwa vikiwaathiri zaidi kina mama na kama wasipopata tiba mapema kuna uwezekano wa kuathiriwa zaidi katika mifumo ya uzazi.
TBS pekee  haiwezi kufanikisha suala hilo ingawa wanashirikiana na vyombo vya dola lakini kubwa linalohitajika ni kuwepo kwa ushirikiano na Watanzania hasa wafanyabiashara wa nguo hizo.
Hilo likifanyika na wananchi wakielewe madhara yake operesheni ya kutokomeza nguo za ndani za mitumba itafanikiwa.

No comments:

Post a Comment