Thursday, 21 August 2014

Alikiba azungumzia uwezekano wa kufanya wimbo na Diamond Platnumz

Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia. Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM Jana August 20, 2014. Alikiba amesema upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko. 

*Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hichi kitu kipo. Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko na hili liende beach, vazi hili la mpirani, vazi hili la ofisini, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwasababu yeye anafanya kazi nzuri,* alisema AliKiba

Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show na Diamond alijibu kwa kicheko:
*Wewe hujui kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha*

Follow me on Instagram
@omaryramsey 

1 comment:

Anonymous said...

aseee ni sheeedah

Post a Comment