Young Killer Msodoki, Mshindi wa KTMA 2014 aliwasurprise wakazi wa jiji
la Mwanza baada ya kupanda jukwaani na mama yake mzazi katika show ya
Kili Music Tour. Rapper huyo ambaye Mwanza ni nyumbani kwao amekiambia
kipindi cha The Jump Off cha 100.5 sababu iliyompelekea kupanda jukwaani
hapo na bi mkubwa wake.
“Ilikuwa ni moja ya Surprise kwa sababu ujue toka siku niliyochukua tuzo
nilishindwa hata kuongea, so bi mkubwa wangu alikuwa na mengi sana ya
kuzungumza na mashabiki wangu wale ambao wamenifanya mpaka nimefika
hapa.
“Kwa hiyo atayawakilisha wapi yale aliyokuwa nayo moyoni. So, nikaona
nafasi pekee ambayo anaweza akafanya nikupanda nae stejini na kuongea
dukuduku lake lote na kuwapongeza mashabiki waliokuwa wananikubali na
kunisapoti mpaka nikafika pale.”

No comments:
Post a Comment